Sudani

Walinda amani wa umoja wa mataifa waonya kuhusu hali mbaya ya usalama katika jimbo la Jonglei Sudani Kusini

Walinda amani wa umoja wa matifa nchini Sudani Kusini (UNMISS)
Walinda amani wa umoja wa matifa nchini Sudani Kusini (UNMISS) reliefweb.int

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba ghasia na uporaji katika mji wa Pibor kwenye jimbo lenye mgogoro la Jonglei huko Sudan Kusini zimeendelea kuwa mbaya huku kukiwa na mapigano ya waasi na jeshi.

Matangazo ya kibiashara

Walinda amani hao wa umoja wa mataifa wenye kibarua nchini Sudani kusini(UNMISS) wamesema wana wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama ndani na kuzunguka mji wa Pibor siku mbili baada ya watu wenye silaha kuripoitwa kupora hospitalini.

Umoja wa Mataifa umelaani vikali vurugu hizo, uporaji na kuwaondoa katika makazi yao raia na mashirika ya kibinadamu, na kubainisha kuwa umeshitushwa sana na ripoti ya utovu wa nidhamu na kuhusika kwa baadhi ya wanachama wa vikosi vya usalama.

Waasi wa Sudan Kusini ambao waliingizwa rasmi katika jeshi la nchi hiyo wamekuwa wakipigana kumaliza uasi katika mji wa Pibor katika jimbo la Jonglei.