LIBYA

Kituo cha polisi mjini Benghazi chavamiwa na kuchomwa moto

Kituo cha polisi cha mjini Benghaz kikiteketea kwa moto
Kituo cha polisi cha mjini Benghaz kikiteketea kwa moto Presstv.ir

Watu wenye silaha wamevamia na kuchoma moto kituo cha polisi katika mji wa Mashariki mwa Benghazi nchini Libya leo Jumatano wakilipiza kisasi dhidi ya kifo cha mwenzao katika tukio la usiku wa kuamkia leo, afisa usalama amesema. 

Matangazo ya kibiashara

Polisi wameondoka katika kituo cha polisi cha Alhadek ambacho kilichomwa moto na washambuliaji hao, huku risasi zikiendelea kurindima kuzunguka jengo hilo.

Tukio hilo la leo limetokea ikiwa ni saa chache baada ya kundi hilo kujaribu kulipiga mawe jengo hilo usiku wa manane ambapo hata hivyo vikosi vya usalama vilijitahidi kulinda jengo hilo na kufanikiwa kumwua mtu mmoja miongoni mwa wavamizi .

Tukio hilo linakuja siku mbili baada ya gari kulipuka katika mji na kuua watu watatu na kujeruhi wengine 14 tukio ambalo mamlaka nchini Libya ilililaani na kusema kuwa ni tukio la kigaidi lakini baadaye hapo jana uchunguzi ukabainisha kuwa tukio hilo ni ajali.