NIGERIA

Rais wa Nigeria atangaza hali ya hatari katika majimbo matatu nchini humo

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amelazimika kutangaza hali ya hatari katika majimbo matatu nchini humo kutokana na kuendelea kutekelezwa kwa mauaji yanayoendeshwa na kundi la Boko Haram. 

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan nationalmirroronline.net
Matangazo ya kibiashara

Rais Jonathan ametangaza hali hiyo ya hatari na kumuagiza mkuu wa majeshi kupeleka wanajeshi zaidi katika maeneo hayo ambayo amesema hali yake ya usalama imezidi kuzorota katika siku za karibuni.

Kiongozi huyo wa Nigeria amesema watahakikisha wanawasaka wanamgambo na magaidi wanaofanya mauaji hayo popote walipojificha na watawafikisha mbele ya vyombo vya sheria kukabiliana na makosa yao.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Nigeria kutangaza hali ya hatari tangu kuzuka kwa kundi la Boko Haram mnamo mwaka elfu mbili na tisa na kuendesha mashambulizi wakipinga utolewaji wa elimu ya Magharibi.