SOMALIA

Mbabe wa kivita ajitangaza rais wa eneo lililojitangazia uhuru wake la Jubaland nchini Somalia

Eneo lililojitangazia uhuru la Jubaland
Eneo lililojitangazia uhuru la Jubaland geesguud.com

Mbabe wa kivita katika eneo la Jubaland Kusini mwa Somalia amejitangaza kuwa rais wa eneo hilo ambalo lilitangaza kujitenga, viongozi wa jadi wamesema muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwa kamanda mwingine wa kijeshi katika nafasi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Huku mvutano ukiwa juu , hatua hiyo imeongeza hatari ya machafuko baina ya makundi hayo hasimu Kusini mwa mji wa bandari wa Kismayo , ngome ya kale ya wapiganaji wa Al Shabab ambako majeshi ya Kenya chini ya majeshi ya Umoja wa Afrika yamepiga kambi kwa sasa.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mji huo ulikuwa tulivu leo Alhamisi , lakini wakazi wa eneo hilo wameripoti kuwa wanamgambo wa jadi wanaimarisha nafasi zao katika eneo lote la Kismayo.

Jana Jumatano mbabe wa kivita Ahmed Madobe alichaguliwa kuwa rais wa eneo hilo la Jubaland kwa mkutano wa viongozi wapatao 500 na viongozi wa jadi.