MISRI

Mamia waandamana Misri kupinga utawala wa Morsi

Waandamanji nchini Misri
Waandamanji nchini Misri english.ahram.org.eg

Mamia ya watu wameandamana katika bustani ya Tahrir jijini Cairo Misri leo Ijumaa wakimtaka rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi kujiuzulu na kudai ufanyike uchaguzi wa mapema vyombo vya habari nchini humo vimearifu. 

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yaliitishwa na makundi kadhaa ya upinzani, ikiwa ni pamoja na chama cha Al-Dustur cha kiongozi wa zamani wa taasisi ya umoja wa mataifa ya uangalizi wa nguvu za Atomic Mohamed ElBaradei na kile cha harakati za Aprili 6 ambacho kiliongoza uasi wa mwaka 2011 uliomwondoa madarakani rais Hosni Mubarak.

Maandamano yalianzia maeneo mbalimbali ya mji mkuu na yalilenga kuwakutanisha kwenye uwanda wa Tahrir eneo ambalo limekuwa kitovu cha mapambano dhidi ya Mubarak.

Katika moja ya maandamano hayo watu walibeba mabango makubwa mawili moja likisomeka kuwa “uchaguzi wa mapema wa rais”, na lingine likiandikwa “katiba inayowaunganisha wamisri” kwa maana ya kuwa wanhitaji mambo hayo kutekelezwa.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa hali ya usalama imeimarishwa kuzunguka wizara ya mambo ya ndani, karibu na uwanda wa Tahrir, eneo ambalo limekuwa chachu ya vurugu kwa kipindi kilichopita.