Mali yahitaji msaada zaidi wa kibinadamu
Mke wa rais wa Ufaransa bi Valerie Trierweiler amesema kuwa ameguswa sana na hali ya mambo nchini Mali baada ya kukamilisha ziara yake ya saa 48 katika taifa hilo lenye vita na koloni la kale la nchi yake.
Imechapishwa:
Mke huyo wa Rais Francois Hollande, ametembelea nchini Mali kama sehemu ya utume kwa ajili ya watoto na wanawake na alitembelea wagonjwa hospitalini na watoto wa shule, akielezea jukumu muhimu la askari wa kike katika kuleta amani.
Bi Valerie ameelza kuwa kamwe hatosahau ziara hiyo kutokana na kwamba amebaini ukubwa wa tatizo la Mali kinyume na inavyodhaniwa na akaongeza kuwa Mali inahitaji vitu vingi vya misaada ya kibinadamu.