KENYA

Rais Kenyatta awaonya wahujumu usalama

Rais wa Kenya Uhuru Mwigai Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Mwigai Kenyatta talkradionews.com

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa onyo kali kwa wanaohujumu usalama katika taifa hilo ambalo limeshuhudia utovu wa usalama kwa siku za hivi karibuni, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha yao. 

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya rais Kenyatta imekuja kufuatia kashfa dhidi ya serikali yake kushindwa kudhibiti hali ya usalama ambapo amesema kuwa serikali itahakikisha inawatia hatiani wale wote wanaohusika na kuhujumu usalama.

Siku kudhaa zilizopita machafuko yameshuhudiwa Kaskazini mwa taifa hilo huku mashambulizi yakizidi katika eneo la Magharibi jambo linalotishia usalama wa taifa hilo huku mamlaka husika zikitajwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Hapo jana watuhumiwa wawili wa ugaidi wameuwawa na polisi katika mtaa wa Githurai jijini Nairobi, baada ya kuishi nchi humo kwa muda wa miezi miwili bila mamlaka za usalama kufahamu kuhusu uwepo wao.