Sudani

Watu 29 wauwawa katika mapigano ya koo Sudani Kusini

Kijana wa jamii ya wafugaji akiwa na mifugo huko Sudani Kusini
Kijana wa jamii ya wafugaji akiwa na mifugo huko Sudani Kusini tvcnews.tv

Watu zaidi ya ishirini na tisa wameripotiwa kupoteza maisha nchini Sudan Kusini kufuatia mapigano ya koo za wafugaji na wakulima kaskazini mwa jimbo la Upper Nile na Jonglei. 

Matangazo ya kibiashara

Polisi kwenye jimbo hilo wamesema kuwa watu wenye silaha walivamia mji wa Tolleri na kuanza kuwashambulia wenyeji wake na kuua watu zaidi ya 23, mauaji ambayo polisi wanasema yamezua hofu kwa wananchi wa maeneo hayo.

Miongoni mwa waliouwawa ni pamoja na wanawake 11 na watoto wannena watu wengine 17 wamejeruhiwa ambapo shirika la msaada la madaktari wasio na mipaka walisafiri kwa boti iendayo kasi hadi eneo la tukio na kuchukua majeruhi 16 na kuwapeleka katika hospitali yao ya mjini Nasir.

Jumuiya ya kimataifa imeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa machafuko kwenye jimbo la Jonglei ambako makundi ya waasi yameendelea kutekeleza vitendo vya uporaji.