MADAGASCAR

Ban awataka mahasimu wa Madagascar kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kulmiyenews.com

Umoja wa Mataifa umekashifu vikali hatua ya kupitishwa kama wagombea urais, Andry Rajoelina rais wa kipindi cha mpito nchini Madagascar, na Didier Ratsira rais wa zamani wa nchi hiyo, pamoja na Lalao Ravalomanana kuwania uchaguzi mkuu nchini humo.  

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anatiwa wasiwasi kama vile jamii ya kiuchumi ya mataifa ya nchi za magharibi mwa Afrika na Kusini SADC juu ya mvutano wa kisiasa.

Kulingana na taarifa hiyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameghadhabishwa na hatuwa hiyo na kuwataka viongozi hao kuheshimu maamuzi ya viongozi wa SADC ambao waliwataka viongozi hao kukaa kando kuacha nafsi kwa viongozi wengine kuwania nafasi hiyo.

Aidha Umoja huo umetishia kusitisha msaada wake katika mchakato wa uchaguzi huo ikiwa wagombea hao hawatajiondoa katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.