SOKA

Droo ya vilabu vya soka kanda ya CECAFA yatolewa

Katibu mkuu wa CECAFA Nicolas Musonye
Katibu mkuu wa CECAFA Nicolas Musonye sodere.com

Mabingwa watetezi wa taji la Kagame katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA Yanga ya Tanzania imejumuishwa katika kundi la tatu pamoja na Express ya Uganda,Ports ya Djibouti na Vitalo la Burundi. 

Matangazo ya kibiashara

Droo ya mashindano haya imefanyika leo Jumannne jijini khartoum huku kundi weyeji ,Al Hilal Kadugli,Al Nasir, Falcons, Al Ahly Shandy pamoja na Tusker ya Kenya.,

Simba ya Tanzania iko katika kundi la A pampja na Merriekh El Fasher, pia ya Sudan,APR ya Rwanda na Elman ya Somalia.

Makala ya mwaka huu yatafanyika kati ya Juni 18 na Julai tarehe katika jimbo la Darfur na Kordofan Kusini.

Itakuwa mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa ya soka katika kanda ya Afrika Mashariki kuandaliwa katika majimbo hayo.

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolas Musonye amesema maandalizi ya mashindnao hayo yamekamilika katika viwanja vyote katika majimbo hayo.