TOGO

Kocha wa Togo atishia kujiuzulu

Kocha wa Togo Didier Six
Kocha wa Togo Didier Six rfi.fr

Kocha wa Togo Didier Six ametoa siku nane kwa shirikisho la soka nchini humo kumrejeshea gharama za usafiri zenye thamani ya Euro laki moja la sivyo atajiuzulu nafasi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo mfaransa ameweka wazi kuwa aligharamia wafanyakazi wake kwa pesa yake binafsi wakati wasafari zao mbalimbali kusaka wachezaji wa kimataifa wa Togo na hadi sasa bado hajarejeshewa fedha hizo.

Hapo awali shirikisho la soka nchi humo lilisema kuwa halitambui chochote kuhusu gharama hizo na kwamba haliwezi kulipa madai yasiyotambulika.

Tishio la Didier kuachia ngazi linakuja yakiwa yamesalia majuma mawili pekee kabla Sparrow Hawks wamenyane na Cameroon Juni 9 na karibu mwezi mmoja kabla ya kukutana na Libya Juni 14.

Six aliazna mgomo binafsi siku mbili zilizopita kudai malipo yake na anasema kwamba hatatoa orodha yoyote ya wachezaji kwa ajili ya kukutana na timu zilizotajwa mpaka hapo atakapolipwa.

Ikiwa na alama moja mkononi iliyopatikana katika michezo mitatu, nafasi ya Togo kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2014 ni ndogo katika kundi I linaloongozwa na Cameroon yenye alama sita, ikifuatiwa na Libya yenye alama tano na DR Congo yenye alama nne.