DRC-RWANDA

Ban Ki Moon asema Rwanda ni muhimu katika utatuzi wa mzozo wa DRCongo

Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa UN Ban Ki Moon REUTERS/Alain Amontchi

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa Rwanda ni nchini muhimu katika kuhakikisha amani inapatikana katika eneo tete la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. 

Matangazo ya kibiashara

Ban ametoa kauli hiyo jana Ijumaa wakati alipotembelea eneo hilo kikiwa ni jitihada za kuongeza nguvu kwenye mkataba mpya wa kukomesha vurugu zilizodumu kwa miongo kadhaa.

Aidha Ban amesema kuwa kikosi maalum kinatarijiwa kuanza operesheni zake huko Mashariki mwa DR Congo hivi karibuni huku rais wa benki kuu Jim Yong Kim akitoa dola bilioni moja za kuimarisha usalama kwenye kanda ya maziwa makuu,

Mkataba wa Umoja wa Mataifa uliotiwa saini mwezi Februari na nchi 11 za ukanda huo baada ya mapigano ya umwagaji damu yaliyotekelezwa na waasi wa M23 wa nchini DRCongo,unalenga kukomesha vita vya muda mrefu katika eneo lenye utajiri wa madini Mashariki mwa Kongo, ambalo ni jirani Rwanda.