MALI

Raia wa Mali watolewa wito kuwa katika hali ya utulivu wakati wakielekea kwenye uchaguzi nchini humo

Waasi wa Tuareg waliokuwa wakipambana na Vikosi vya Serikali na kigeni Kaskazini mwa Mali
Waasi wa Tuareg waliokuwa wakipambana na Vikosi vya Serikali na kigeni Kaskazini mwa Mali

Mjumbe wa Upatanishi katika Mazungumzo ya kuleta amani nchini Mali ametaka Raia nchini humo kuwa Watulivu wakati huu ambapo kumekuwepo na ukosoaji mkubwa kuhusu Makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Serikali na Waasi.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano ya Ouagadougou, yaliyofikiwa siku ya Jumanne baada ya siku 10 za Mazungumzo nchini Burkinafaso, utawezesha Vikosi vya Mali kuingia katika Mji wa Kidal unaodhibitiwa na Wanamgambo wa Tuareg.
 

Serikali ya Mali ilitia saini Makubaliano ya amani na Wanamgambo wa MNLA na Tuareg nchini Burkina Faso, Pnde hizo zilikubali kuacha mapigano na kuandaa mazungumzo ya Amani baada ya Uchaguzi.
 

Raia wa Mali wameunga Mkono Makubaliano hayo lakini Wachambuzi wa mambo wamekuwa na hofu juu ya Utekelezwaji wa Makubaliano hayo, hasa juu ya usimamizi thabiti katika utekelezaji wa Maazimio.
 

Rais wa Mali Dioncunda Traore amefanya mikutano kadhaa na Viongozi wa Vyama vya siasa kuwaeleza juu ya Makubaliano ya Ouagoudougou wakati huu wakielekea katika Uchaguzi.

Wananchi wa Mali wanatarajiwa kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Urais uliopangwa kufanyika tarehe ishirini na nane mwezi Julai kwa lengo la kumaliza serikali ya muda iliyokaa madarakani ili kurejesha hali ya utulivu.