TANZANIA-MAREKANI

Obama kuwasili Tanzania hii leo kwa ziara ya siku mbili

Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete libya360.wordpress.com

Rais wa Marekani Barack Obama anawasili nchini Tanzania leo Jumatatu, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Akiwa nchini Tanzania rais Obama atafanya mazungumzo na rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete  na waandishi wa habari na kisha kutembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme Barabi Afrika.

Mpango huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.

Aidha Obama ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.

Katika ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani