CHAD

Rais wa zamani wa Chad akamatwa nchini Senegal

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre
Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre sweetcrudereports.com

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre amekamatwa jana Jumapili nchini Senegal akikabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati alipokuwa madarakani kati ya mwaka 1982 na 1990.

Matangazo ya kibiashara

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa zaidi ya watu elfu arobaini waliuawa nchini Chad chini ya utawala wake.

Habre ambaye amekuwa akiishi uhamishoni nchini Senegal kwa takribani miaka ishirini na miwili atafikishwa mahakamani katika mahakama maalumu nchini Senegal iliyoanzishwa kwa makubaliano kati ya serikali ya Senegal na Umoja wa Afrika AU.

Mashtaka dhidi ya kiongozi huyo yatakuwa ya kihistoria barani Afrika kwani viongozi wengi wanaokabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita wamekuwa wakishitakiwa katika mahakama za kimataifa.