ZIMBABWE

Mahakama Zimbabwe yaamuru uchaguzi mkuu kufanyika Julai 31 kama ilivyopangwa awali

REUTERS/Philimon Bulawayo

Mahakama Kuu ya Zimbabwe imekubaliana na ombi la Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na sasa imemua uchaguzi mkuu nchini humo ufanyike mwinshoni mwa mwezi huu yaani Julai 31 kama ilivyopangwa awali.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama nchini Zimbabweimetoa uamuzi huo baada ya kusikiliza ombi la rais Robert Mugabe la kutaka uchaguzi Mkuu nchini humo kuahirishwa kwa wiki mbili zaidi.

Mugabe alifika Mahakamani baada ya shinikzo kutoka kwa Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na viongozi wa mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC kutaka uchaguzi huo akuahirishwa ili kuruhusu mabadiliko katika taasisis mbalimbali nchini humo.

Tsvangirai amabye anataka uchaguzi kufanyika mwezi Oktoba anasema uchaguzi ulio huru na haki unaweza kufanyika nchini humo baada ya mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari, tume ya uchaguzi na vyombo vya ulinzi nchini humo.

Waziri mkuu huyo wa Zimbabwe amesema kuwa uchaguzi huo unapaswa kufanyika baada mabadiliko ya katiba mpya kutekelezwa katika mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Mapendekezo hayo yalipingwa vikali na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye ameshikilia msimamo wake hali ambayo imekosolewa na jumuiya kimataifa.