Senegal

Serikali na upinzani nchini Guinea wakubaliana kuhusu uchaguzi wa wabunge

RFI

Upinzani nchini Guinea na Chama tawala nchini humo wamefikia makubaliano kufanya uchaguzi wa wabunge mwezi Septemba, mwaka huu na hivyo kuashiria kumalizika kwa mvutano uliokuwepo baina ya pande hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kutia saini makubaliano yao hapo jana chini ya uangalizi wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa Muungano wa Vyama vya upinzani nchini humo, Aboubacar Sylla amesema kuwa wamekubaliana mambo kadhaa yakiwemo kuipa kandarasi kampuni moja kutoka Afrika kusini kwa ajili ya kutangeneza vitambulisho vya wapiga kura.

Awali upinzani nchini Senegal ulidai kuwa kampuni hiyo ina maslahi na chama tawala tuhuma ambazo zilikanushwa na chama tawala.

Guinea ilifanya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2010, ingawa uchaguzi huo ulielezwa kufanyika kwa uwazi, kura hizo zilitawaliwa na mgawanyiko wa kikabila kati ya jamii ya Malinke na Peul.

Kabila la Malinke linamuunga mkono Alpha Conde huku jamii ya Peul inamuunga mkono Cellou Dalein Diallo.