NIGERIA

Umoja wa Ulaya, EU wakemea Shambulio dhidi ya Wanafunzi Kaskazini mwa Nigeria

Kiongozi wa Sera za Mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton
Kiongozi wa Sera za Mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton

Umoja wa Ulaya imekemea kile walichokiita mauaji ya kutisha yaliyotekelezwa na Magaidi dhidi ya Watu, hususan Wanafunzi,katika Shambulio dhidi ya Shule ya Sekondari nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Kiislamu lenye msimamo mkali, Boko Haram, lilitokea mwishoni mwa juma lililopita mjini Mamudo na Yobe, jimbo mojawapo kati ya Majimbo matatu ambayo Serikali ilitangaza hali ya hatari Mwezi Mei.
 

Mkuu wa Sera za Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, EU, Catherine Ashton amesema kuwa anakemea mauaji ya Watoto wasio na hatia 30 na Mwalimu wao tukio lililotokea siku ya Jumamosi juma lililopita mjini Mamudo mji ulio Kaskazini mwa Nigeria.
 

Ashton amewaahidi Raia wa Nigeria kushirikiana nao katika kudumisha hali ya usalama, amani na maridhiano kaskazini mwa nchi hiyo, na kutoa wito kwa waliohusika kufikishwa mbele ya vyombo vya Sheria.
 

Manusura wa Shambulio hilo wamesema kuwa Watu wenye silaha waliwazunguka Wanafunzi na Wafanyakazi katika shule moja kaskazini mwa nchi hiyo kisha kuwaweka bwenini kabla ya kuwashambulia kwa milipuko.
 

Kundi la Boko Haram jina linalomaanisha “Elimu ya Magharibi ni dhambi” limeua mamia ya Wanafunzi katika mashambulizi kwenye Shule mbalimbali miezi ya hivi karibuni.