Misri

Kiongozi wa mpito nchini Misri atangaza kuitisha uchaguzi mwanzoni mwa Mwaka ujao

Kiongozi wa Mpito nchini Misri, Adly Mansour
Kiongozi wa Mpito nchini Misri, Adly Mansour Reuters/Amr Abdallah Dalsh

Kiongozi wa mpito nchini Misri ameahidi kuitisha uchaguzi mpya mwanzoni mwa mwaka ujao, baada ya takriban watu 51 wengi wao, wengi wao Wafuasi wa Kiongozi aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi kuuawa nje ya Kambi ya Jeshi jijini Cairo jana.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa mpito, Adly Mansour anatarajiwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Misri halikadhalika mchakato wa kupiga kura ya maoni kwa ajili ya mabadiliko ya Katiba.
 

Chama cha Morsi, Muslim Brotherhood, kilichoongoza maandamano dhidi ya Jeshi na Mapinduzi dhidi ya Kiongozi wao, wametupa lawama kuwa Jeshi na Polisi wamepoteza maisha ya Watu hasa wafuasi wa Chama chao.
 

Jeshi nalo limetupa lawama kwa makundi waliyoyaita ya kigaidi, chama cha upinzani Freedom and Justice, FJP kimetoa wito wa kupinga wale wote wanaojaribu kuiba mapinduzi yao kwa nguvu.
 

Chama hicho kimeiomba jumuia ya kimataifa kuingilia kati kuhakikisha mauaji yanakoma nchini humo na kuzuia hali ya mambo kuwa mbaya zaidi kama ilivyo nchini Syria.
 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amekemea mauaji yaliyotokea nchini Misri na kutoa wito kufanyika uchunguzi ulio huru ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya Sheria waliohusika.