AFRIKA KUSINI

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma afanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

Rais wa Afrika kusini, Jackob Zuma
Rais wa Afrika kusini, Jackob Zuma REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma amefanya mabadiliko kwenye Baraza lake la awaziri kwa mara ya nne akiwaweka kando mawaziri watatu akiwemo Mwanaharakati wa siku nyingi dhidi ya ubaguzi wa rangi na mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Zuma.

Matangazo ya kibiashara

Tokyo Sexwale, aliyekuwa Waziri wa Makazi, amefukuzwa kazi jana sambamba na Waziri wa Mawasiliano Dina Pule na Waziri wa Utamaduni Richard Baloyi.
 

Mabdiliko hayo yalitangazwa ikiwa ni Chini ya Mwaka mmoja kabla Zuma hajatafuta kuliongoza Taifa hilo kwa kipindi kingine cha miaka mitano, pia kufuatia kukosolewa kwa namna anavyoshughulikia maswala ya kiuchumi nchini humo.
 

Sexwale, Mfanyabiashara mkubwa nchini Afrika kusini, alifungwa katika Jela ya kisiwa cha Robben kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa hilo, Nelson Mandela.
 

Pia ni mmoja wa wafuasi wa Chama cha ANC waliokuwa na mpango wa kumpiku Zuma katika Harakati za Uongozi mwaka Jana.
 

Zuma anakabiliwa na Shutma katika mahakama ya kikatiba kwa kushindwa kumteua Mwenyekiti wa kudumu wa Mamlaka ,ambayo kwa hatua ya kukanganya ilitupilia mbali shutma za rushwa dhidi ya Zuma muda mfupi kabla ya kuwa Rais wa Afrika kusini.