MISRI

Utawala mpya nchini Misri waendelea na michakato ya uundwaji wa Serikali mpya

Waziri Mkuu mpya nchini Misri, Hazem el-Beblawi
Waziri Mkuu mpya nchini Misri, Hazem el-Beblawi

Utawala mpya nchini Misri unaendelea na michakato ya kuunda Serikali mpya huku Polisi wakimsaka Kiongozi wa Chama cha kiislamu, Muslim Brotherhood.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Mohamed Morsi kilikataa kuwa Sehemu ya Serikali ya Mpito ambapo Waziri Mkuu Hazem al-Bebawi alitangaza kutoa nafasi za uwaziri kwa Chama hicho.
 

Chama cha Muslim Brotherhood kimeitisha Maandamano siku ya ijumaa kupinga Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Mohamed Morsi.
 

Baada ya mwaka mmoja wa Morsi kuwa madarakani, Chama cha Muslim Brotherhood kiko katika hali tata baada ya sehemu kubwa ya Viongozi wa utawala wa Chama hicho kukamatwa.
 

Polisi hivi sasa wanamsaka Kiongozi wa juu wa Chama hicho, Mohamed Badie baada ya amri kutolewa siku ya jumatano, akishutumiwa kuchochea machafuko jijini Cairo.
 

Badie na Viongozi wenzake wanatafutwa wakishukiwa kuchochea mapigano siku ya jumatatu na kusababisha Watu 53 wengi wao Wafuasi wa Morsi.
 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje Badr Abdelatty amesema kuwa Morsi yuko salama na hashutumiwi kwa kosa lolote mpaka sasa.
 

Hata hivyo vyanzo vya habari za jeshi na Mahakama vimesema kuwa kiongozi huyo huenda akawa na mashtaka ya kujibu.
 

Maelfu ya Wafuasi wa Morsi walikita Kambi nje ya Msikiti jijini Cairo, wakiapa kuondoka mahali hapo ikiwa Morsi atarejeshwa mahakamani.