Zimbabwe

SADC na AU zatakiwa kuhakikisha uchaguzi wa Amani unafanyika nchini humo

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Reuters/Philimon Bulwayo

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Duniani la Amnesty International limetoa wito kwa Umoja wa Afrika AU na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kuhakikisha uchaguzi nchini Zimbabwe unakuwa wa amani.

Matangazo ya kibiashara

Amnesty International kwenye ripoti yake imeamua kuziangukia SADC na Umoja wa Afrika AU kutokana na kuhofiwa machafuko na mgororo uliotokea wakati wa uchaguzi wa mwaka 2008 ukajirudia.
 

Naibu Mkurugenzi wa Amnesty international Barani Afrika Noel Kututwa amekiri kumekuwa na wasiwasi mkubwa wa Taifa za Zimbabwe kuingia kwenye machafuko kipindi hiki Rais Robert Gabriel Mugabe akiendelea na kampeni zake.
 

Vikosi vya Usalama vya Zimbabe vilishutumiwa kukiuka haki za binaadam kwa kuwatisha Wapinzani wa Rais Robert Mugabe huku kukiwa na riopti kuwa Watu 200 waliuawa kwenye uchaguzi wa mwaka 2008 ambapo Mugabe alichuana na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.
 

Maelfu wanaelezwa kupata mateso na kupigwa wakati wa Machafuko ya kisiasa yaliyokumba Zimbabwe.
 

Mwezi Machi, Raia wa Zimbabwe walipiga kura kuunga mkono Katiba mpya ambayo imefungua milango ya kufanyika kwa Uchaguzi.