TUNISIA

Uchaguzi mkuu wa Tunisia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu

REUTERS/Zoubeir Souissi

Waziri Mkuu wa Tunisia Ali Larayedh ametangaza kuwa uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 17 mwezi Desemba baada ya mkutano wa dharura kufanyika zikiwa ni harakati za kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo, huku Waandamanaji nao wakiendelea na harakati zao za kukitaka Chama tawala cha Ennahda kuondoka madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Larayedh ametoa tangazo la uchaguzi baada ya kukutana na Mawaziri na kukutana na Viongozi wanaoshughulikia usalama wa Taifa, mkutano ulioongozwa na Rais Moncef Marzouki.

Hivi sasa yanasubiriwa mabadiliko kadhaa ya vifungu vya katiba ambavyo vinatarajiwa kuwa tayari tarehe 23 mwezi Oktoba huku Larayedh akisema kuwa asilimia 80 ya shughuli za kupata katiba mpya zimekamilika.

Siku ya jumatatu polisi nchini humo walailazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji katika barabara za mji wa Sidi Bouzid wanaondamana kutaka serikali ya Kiislamu kuondoka madarakani.

Maandamano hayo yamechochewa na na mauaji ya kiongozi wa upinzani Mohammed Brahmi aliyeuawa juma lililopita.

Mohammed Brahmi ni kiongozi wa pili wa upinzani nchini humo kuuawa baada ya kiongozi mwingine Chokri Belaid kupigwa risaisi na kuuawa nyumbani kwake mapema mwaka huu.

Upinzani nchini Tunisia umeendelea kuitumu serikali kwa kuwauawa viongozi wao tuhma ambazo serikali imeendelea kukanusha.