MALI

Boubacar Keita awaomba raia wa Mali kumpigia kura nyingi kwenye duru la pili la uchaguzi Agosti 11

waziri mkuu wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta
waziri mkuu wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta REUTERS/Joe Penney

Mshindi wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Mali Ibrahim Boubacar Keita amewataka wananchi nchini humo kumpoigia kura na kumpa ushindi mkubwa wakati wa duru la pili tarehe 11 mwezi huu. 

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu huyo wa zamani ameongeza kuwa ushindi mkubwa utazuia kura zake kuibiwa, huku akisisitiza kuwa kuharibika kwa zaidi ya kura laki nne lilikuwa jambo la kushangaza wakati wa duru ya kwanza.

Uchaguzi huo wa Mali tayari umepangwa kufanyika kwa awamu ya pili mnamo Agosti 11 bada ya mshindi kutopatikana katika duru ya kwanza ambapo waziri mkuu wa zamani Keita aliongoza kwa asilimia 39.2 ya kura zilizopigwa na kufuatiwa na mpinzani wake Soumaila Cisse ambaye alipata asilimia 19.4.

Hata hivyo Cisse ameishutumu serikali kwa kuruhusu udanganyifu mkubwa baada ya wizara ya mambo ya ndani kuseama karatasi za kupigia kura zaidi ya laki nne ziliharibika nje ya kura milioni 3.5 zilizopigwa.