Marekani

Marekani yasisitiza kuendelea kufunga baadhi ya balozi zake Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati

Wanamgambo wa kundi la Al Qaeda linaloitishia Marekani
Wanamgambo wa kundi la Al Qaeda linaloitishia Marekani foreignpolicy.com

Marekani inasema itaendelea kufunga balozi zake Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya kati hadi siku ya Jumamosi kwa hofu ya kushambuliwa na Al-Qeada.

Matangazo ya kibiashara

Balozi 21 zimefungwa tangu Jumapili baada ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kutangaza kuwa kundi la Al Qaeda lilikuwa linajiandaa kufanya mashambulizi.

Marekani imewataka raia wake kuepuka kusafiri Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati hadi pale watakapopewa maelezo zaidi.

Hata hivyo Marekani imesema kuwa itafungua balozi zake nchini Algeria, Afghanistan na Iraq leo Jumatatu.

Uingereza nayo imejiunga na Marekani kufunga ubalozi wake jijini Sanaa nchini Yemen na kusema kuwa utafunguliwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha Ramadhani.

Mbali na Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, Marekani imeongeza kuwa balozi zake jijini Antananarivo nchini Madagascar, Bujumbura, Djibouti, Khartoum, Kigali na Port Louis nchini Mauritius zitafungwa wiki hii.