MISRI

Ujumbe wa kimataifa waongeza muda wa ziara nchini Misri

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani William Burns
Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani William Burns RFI

Wajumbe wa kimataifa kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya na Qatar, wameongeza muda wa ziara yao nchini Misri wakati juhudi za kutafuta njia ya amani ya kumaliza mzozo uliotokana na jeshi kumwondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Morsi kushika kasi leo Jumatatu. 

Matangazo ya kibiashara

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani William Burns amekutana na naibu wa pili wa rais Morsi, Khairat al-Shater akiwa gerezani, shirika la habari MENA limearifu.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa Burns aliambatana na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Bernardino Leon na wanadiplomasia wa juu wa Qatar na Umoja wa falme za Kiarabu wakati alipomtembelea Shater katika gereza lenye ulinzi mkali la Tora jijini Cairo.

Chanzo kutoka uwanja wa ndege jijini Cairo kimeeleza kuwa Burns na Leon walitatajiwa kuondoka nchini Misri jana usiku lakini wameongeza muda wa kubaki nchini humo.