DRC

Rais Kabila asisitiza haja ya mazungumzo ya kitaifa kuhusu usalama wa DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila forbes.com

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila kwa mara nyingine amesema kuna umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa kujadili hali ya usalama na kisiasa nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Rais Kabila ameisisitiza kuwa mazungumzo hayo yatafanyika hivi karibuni kwa lengo la kuwaleta pamoja wananchi wa taifa hilo.

Hata hivyo vyama vya upinzani nchini humo vinasema mazungumzo hayo hayana maana kwa kuwa mazungumzo mengi yamefanyika bila mafanikio na sasa raia wanahitaji kuona kiongozi atakaye wasimamia vizuri na kuleta usalama badala ya mazungumzo.

Kwa upande wa mashirika ya kiraia nayo yanasema mazungumzo hayo yanasatahili kufanyanyika haraka iwezekanavyo ili kumaliza hali ya wasiwasi Mashariki mwa nchi hiyo