MISRI-AU

Umoja wa Afrika AU wasisitiza kutoirejeshea Misri uanachama mpaka itakapopata rais halali

Mwnyekiti wa umoja wa Afrika Dokta Nkosazana Dlamini-Zuma
Mwnyekiti wa umoja wa Afrika Dokta Nkosazana Dlamini-Zuma Reuters

Umoja wa Afrika unasema hautasitisha marufuku yaliyoiwekea Misri baada ya kuangushwa kwa uongozi wa Mohammed Mosri mwezi uliopita. 

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo ulitolewa jijini Addis Ababa na uongozi wa AU ambao umesema utaitambua Misri baada ya kuwepo kwa rais halali.

Mwenyekiti mkuu wa Umoja huo Nkosazana Dlamini-Dzuma ametangaza kuwa uanachama wa Misri unaweza tu kurudishwa ikiwa uchaguzi huru na wa haki utakaoshirikisha wananchi wa nchi hiyo utafanywa kwa mujibu wa katiba.

Hata hivyo Dlamini-Zuma ametuma ujumbe maalum wa marais wastaafu watatu wa Afrika kwenye mji mkuu wa Misri kuchunguza ikiwa kuna uwezekano wa mabadiliko ya katiba kutokea.

Kutumwa kwa marais hao kunatokana na ombi la watawala wa Misri la kurudishiwa uanachama lililopelekwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika na mwakilishi maalum wa Misri Bi.Mona Omar.

Haya yanajiri wakati maseneta wawili wa Marekani John McCain na Lindsay Graham wako nchini Misri kwa juhudi za serikali ya rais Obama kumaliza mzozo ulioko wa uongozi.