Afrika Kusini

Afya ya Nelson Mandela yaendelea kuimarika

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela wakati akizungumza kwenye moja ya ziara zake
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela wakati akizungumza kwenye moja ya ziara zake Reuters

Afya ya Baba wa Tifa la Afrika kusini, Nelson Mandela imeelezwa kuimarika taratibu ingawa bado yu mahututi, Ofisi ya Rais nchini Afrika kusini imeeleza.

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani na aliyeongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini amekuwa hospitalini kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili akikabiliwa na tatizo la mapafu.
 

Ofisi ya Rais imesema kuwa Mandela anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini jijini Pretoria na Madaktari wamemweleza Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma kuwa Mandela ingawa yuko mahututi lakini amekuwa na maendeleo mazuri.
 

Rais Zuma ametoa wito kwa Raoa wa Afrika kusini kumuombea Mandela arejee katika Afya njema.
 

Rais Zuma ndiye aliye na mamlaka ya kutoa Taarifa juu ya Manendeleo ya Afya ya Mandela na hakuwahi kutoa tena Taarifa yeyote tangu tarehe 31 mwezi Julai.