SUDANI

Watu 150,000 waathiriwa na Mafuriko nchini Sudani

Rais wa  Sudani Omar Hassan Al Bashir
Rais wa Sudani Omar Hassan Al Bashir REUTERS/Afolabi Sotunde

Idadi ya Watu walioathiriwa na Mafuriko mwezi huu nchini Sudani imeongezeka na kufikia Takriban Watu 150,000 na kuwa idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi, Umoja wa Mataifa umeeleza hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya asilimia hamsini ya walioathiriwa, 84,000 wako katika maeneo ya nayoizunguka Khartoum, Shirika la umoja wa Mataifa, linaloratibu misaada ya kibinaadam ,OCHA limeeleza.
 

Shirika la OCHA limesema kuwa mvua zaidi zinatarajiwa kunyehsa siku za usoni na kuwa idadi ya Watakaoathirika itaendelea kuongezeka kadiri mvua zitakavyokuwa zikiendelea kunyesha.
 

Takwimu za Shirika hili zimetolewa baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa ijumaa iliyopita zilizotolewa na mashirika mbalimbali nchini Sudani.
 

Mvua kubwa zilizonyesha ambazo zilisababisha mafuriko zilianza Tarehe 1 mwezi Agosti na kuathiri takriban watu 100,000 katika maeneo kadhaa nchini Sudani.
 

Hapo jana taarifa za nchini humo zilisema kuwa Watu 36 walipoteza maisha katika jimbo la Nile, kaskazini mwa Khartoum.
 

Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine yamekuwa yakitoa misaada ya kibinaadam kama vile mashuka na Maji ya kunywa.