TUNISIA

Mikutano mikubwa yaitishwa na Chama tawala cha Ennahda na Upinzani nchini Tunisia

Mwenyekiti wa Chama tawala nchini Tunisia, Rached Ghannouchi
Mwenyekiti wa Chama tawala nchini Tunisia, Rached Ghannouchi REUTERS/Zoubeir Souissi

Chama tawala cha kiislamu nchini Tunisia,Ennahda na upinzani wameitisha mikutano kila upande kuadhimisha siku ya kitaifa ya Wanawake hii leo, hali ambayo imeendelea kuleta mgawanyiko nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Lakini mazungumzo kati ya mwenyekiti wa chama cha Ennahada na Kiongozi wa shirikisho wa vyama vya Wafanyakazi Houcine Abassi yanalenga kujadili mgogoro unaoendelea nchini Tunisia.

Mgogoro wa kisiasa uliibuka nchini Tunisia baada ya kuuawa kwa Mwanasiasa wa upinzani mwezi uliopita.
 

Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi, ambalo limekuwa likiunga mkono baadhi ya matakwa ya upinzani nchini Tunisia limekuwa kikionekana kuwa msuluhishi wa mgogoro kati ya Serikali na upinzani nchini Tunisia.
 

Wakosoaji wa Serikali wameitisha maandamano hii leo jioni kwa lengo la kutetea haki za Wanawake baada ya kupiga kambi nje ya Jengo la Bunge, ambapo upinzani ulikuwa ukikemea mauaji ya julai 25 dhidi ya Mbunge wa Upinzani Mohamed Brahmi.
 

Wakosoaji wa chama cha Ennahda kikiwemo shirikisho la vyama vya Wafanyakazi UGTT wanadai kuwa haki za Wanawake zinakabiliwa na tishio kubwa kutoka katika Serikali ya Chama cha Ennahda.