NIGERIA

Watu 56 wauawa na Watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Wanajeshi wa usalama wakishuhudia madhara ya tukio la mashambulizi ya Boko Haram
Wanajeshi wa usalama wakishuhudia madhara ya tukio la mashambulizi ya Boko Haram Reuters/Afolabi Sotunde

Waumini wa kiislamu 44 wameuawa kwa risasi na Watu wanaodhaniwa kuwa Waislamu wenye msimamo mkali walipovamia msikiti ambao waumini hao walikuwa wakiabudu mjini Konduga Nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa mwishoni mwa juma yanaaminika kuwa ya kulipiza kisasi dhidi ya hatua iliyochukuliwa na Raia kusaidia Jeshi kupambana na makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali, Boko Haram ambao wamekuwa wakifanya uasi tangu mwaka 2009.

Afisa wa Serikali amesema kuwa Watu hao wenye silaha wanaaminika kuwa kundi la Boko Haram ambao waliwavamia watu waliokuwa wakiabudu ndani ya msikiti na kushambulia kwa risasi iliyoua watu 44.

Watu wengine 12 waliuawa katika kijiji cha Ngom siku ya jumamosi

Machafuko hayo yalikuja baada ya Jeshi nchini humo kuanzisha operesheni kaskazini mashariki mwa Nigeria inayolenga kumaliza uasi nchini humo, pia hali ya hatari iliyotangazwa mwezi mei mjini Konduga.
 

Majuma ya hivi karibuni Jeshi la Nchini humo lilitoa wito wa kuanzisha kwa vikosi kazi kwa ajili ya kusaidia mamlaka kuwanasa wafuasi wa kundi la Boko Haram.
 

Uasi wa Boko haram umegharimu maisha ya watu 3,600 tangu mwaka 2009, pia mauaji ya Vikosi vya usalama, ambao wamekuwa wakishutumiwa kukiuka haki za binaadam.