Misri

Takriban Watu 124 wauawa katika Operesheni za kuwasambaratisha Wafuasi wa Morsi nchini Misri

Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood ,Gehad El-Haddad
Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood ,Gehad El-Haddad Twitter profile

Takriban Watu 124 wameuawa hii leo wakati Polisi ilipokuwa katika Operesheni ya kuwasambaratisha Raia wanaomuunga mkono Kiongozi aliyeondolewa madarakani, Morsi waliokuwa wakiandamana na kuweka Kambi jijini Cairo nchini Misri.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema kuwa miili iliyopatikana katika kambi ya Rabaa al-Adawiya inaashiria kuwa Watu waliuawa kutokana na Majeraha waliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa Risasi.
 

Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema kuwa Askari wake wa usala,a wawili wameuawa wakati wakiwa kwenye Operesheni hiyo.
 

Chama cha Muslim Brotherhood kimewataka Raia wa Misri kuingia mitaani kwa wingi kukemea kile walichodai mauaji dhidi ya Raia.
 

Msemaji wa Chama hicho Gehad al-Haddad ametoa wito huo kupitia ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa operesheni ya vikosi vya usalama hailengi kuwaondoa katika kambi walizozipiga isipokuwa kuwanyamazisha wanaopinga mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Morsi.
 

Vikosi vya usalamavilizingira Watu waliokuwa wamepiga kambi na kutumia gesi ya kutoa machozi wakati wakianza maandamano yao hali iliyowafanya Waandamanaji kusambaa na kukimbia kia mahali.
 

Televisheni ya Taifa ya Misri imesema kuwa Watu kadhaa wamekamatwa mjini Nasr wakiwa na silaha na Mitungi ya Gesi.
 

Wizara ya Mambo ya ndani imethibitisha kukamatwa kwa watu 200, wakiwemo 50 kutoka kmbi ya Adawiyeh mjini Nasri na 150 kutoka kambi ya viwanja vya Nahda mjini Giza.
 

Wizara ya mambo ya ndani imeonya kuwa Vikosi vya usalama vitawawajibisha Waandamanaji wanaokiuka Sheria, na kusema kuwa watahakikisha kuwa wanakuwa salama wale watakao ondoka kwa hiari yao kwenye viwanja hivyo.