Mali

Kiongozi wa Mapinduzi ya nchini Mali dhidi ya Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Amadou Toumani Toure apandishwa Cheo

Kiongozi wa Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Mali, Kepteni  Amadou Sanogo
Kiongozi wa Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Mali, Kepteni Amadou Sanogo AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Mwanajeshi aliyeongoza mapinduzi dhidi ya Serikali ya Mali hatua iliyosababisha kuzuka kwa makundi ya uasi amepandishwa cheo.Serikali imeeleza, ikiwa ni siku kadhaa baada ya kufahamika kwa Rais mpya wa Mali.

Matangazo ya kibiashara

Kepteni Amadou Sanogo aliungana na maafisa wenzie katika Operesheni ya kumuangusha aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Amadou Toumani Toure, tarehe 22 mwezi March mwaka 2012.

Wizara ya ulinzi imesema kuwa Baraza la Mawaziri limeridhia kuteuliwa kwa Kapteni Sanogo kuwa Luteni Jenerali wa Jeshi la Mali siku mbili baada ya Ibrahim Boubacar Keita kuibuka Rais Mteule.
 

Shirika la kimataifa la Waangalizi wa haki za binaadam Humman Rights Watch limesema kuwa kitando cha kumpa cheo Sanogo ni cha aibu.
 

Mtafiti ndani ya Shirika hilo Corinne Dufka,amesema Badala yake Kepteni Sanogo angepaswa kufanyiwa uchunguzi juu ya shutma za kujihusisha na vitendo vya kutesa na kujihusisha na vitendo vingine vya ukiukaji wa haki za binaadam.
 

Sanogo aliongoza mapinduzi dhidi ya Utawala wa Toure akidai kuwa Serikali hiyo haikuwa na uwezo wa kupambana na uasi kaskazini mwa nchi hiyo na kuahidi kuwa atakabidhi madaraka kwa Serikali ya kiraia.