SOMALIA

Majeshi ya AMISOM na ya Somalia yashutumiwa kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji

Wanajeshi wa AMISOM wakiwa nchini Somalia katika Operesheni dhidi ya Al Shabaab
Wanajeshi wa AMISOM wakiwa nchini Somalia katika Operesheni dhidi ya Al Shabaab Reuters/Stuart Price/African Union-UN Information Support Team

Kikosi cha umoja wa Afrika kilicho kwenye Operesheni nchini Somalia kinafanya uchunguzi shutma za vitendo vya ubakaji vilivyofanywa na Wanajeshi kadhaa dhidi ya Mwanamke mmoja, tukio lililoamsha ghadhabu jijini Mogadishu, Umoja wa Afrika umeeleza.

Matangazo ya kibiashara

Mwanamke wa kisomali amedai kuwa alikamatwa, kuburuzwa na kisha kubakwa na Wanajeshi wa Serikali ya Somalia na wa AMISOM.
 

Kikosi cha AMISOM kimekiri kuwa kimepokea shutma hizo dhidi ya Wanajeshi wake.
Kauli ya AMISOM imesema kuwa jeshi lake na lile la Somalia limeandaa kikosi ambacho kitafanya uchunguzi na baadae hatua stahiki zitachukuliwa baada ya kubainika ukweli juu ya shutuma hizo.
 

Majeshi ya Umoja wa Afrika yaliyo kwenye Operesheni nchini Somalia yamekemea vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji.
 

Vikosi vya Umoja wa Afrika vinavyojumuisha Wanajeshi kutoka nchi tano, Burundi, Djibouti, Kenya, Sierra Leone na Uganda vimekuwa vikipambana na Wanamgambo wa Taliban wenye uhusiano na Al-Qaeda, Al Shabaab tangu mwaka 2007.
 

Ikiwa itathibitika kuwa kweli Wanajeshi wa Vikosi hivyo wamejihusisha na vitendo vya ubakaji itaathiri heshima ya Vikosi vya Umoja wa Afrika iliyojiwekea mbele ya uso wa jumuia ya kimataifa.
 

Jeshi la Somalia awali liliwahi kushutumiwa na makundi ya kutetea haki za binaadam kuwa Wanajeshi wake wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Wanawake vikiwemo vitendo vya ubakaji.
 

Shutma juu ya Vitendo vya ubakaji dhidi ya Mwanamama huyo kutekelezwa na Wanajeshi wa AMISOM imewashtua Walio wengi.