SOMALIA

Ugonjwa wa Polio waibuka tena nchini Somalia, wakati huu hali ya usalama ikielezwa kuwa tete

Wafanyakazi wa Shirika la Madaktari wasio namipaka, MSF wakiwa katika kambi ya Dadaab nchini Kenya
Wafanyakazi wa Shirika la Madaktari wasio namipaka, MSF wakiwa katika kambi ya Dadaab nchini Kenya REUTERS/Thomas Mukoya

Wafanyakazi wa Mashirika ya misaada nchini Somalia, wako katika jitihada za kudhibiti virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Polio, wakati huu ambapo hali tete ya usalama inaikabaili nchi hiyo Umoja wa Mataifa umeeleza hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Miaka sita baada ya nchi hiyo iliyo katika eneo la pembe ya Afrika kutangazwa kuwa imefanikiwa kupambana na ugonjwa wa Polio takriban Wagonjwa 105 wamethibitishwa kuugua ugonjwa huo, hali inayoelezwa kuwa mbaya zaidi, Ofisi ya Kuratibu maswala ya kibinaadam, OCHA imeeleza.
 

Wakati watu milioni nne wamepatiwa chanjo ya kudhibiti Polio, na kutoa dawa kwa zaidi ya Watoto 600,000 waishio Kusini na katikati ya Somalia, bado maeneo yanadhibitiwa na Al Shabaab yamekuwa kikwazo kwa jitihada hizo.
 

Taarifa zinasema kutokana na kushindwa kufikiwa kwa jitihada hizi kwa ajili ya utoaji wa Chanjo, Taarifa ya OCHA imesema kwua Somalia inaendelea kuwa eneo gumu na lenye mazingira magumu kwa Wafanyakazi wa Mashirika ya misaada.
 

Wakati zaidi ya Watoto 100 wakiripotiwa kuwa na dalili ya kuathiriwa na Polio bado inaelezwa kuwa kuna dalili ya kuwepo kwa Watoto walioathirika maelfu zaidi ambao hawana dalili bado za ugonjwa huu.
 

Ugonjwa huu pia umeripotiwa kukumba kaskazini mashariki mwa Kenya, ambapo eneo hilo linawatunza Wakimbizi wa Kisomali katika kambi zake.
 

Wakati hali ikiripotiwa kuwa hivyo Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF nalo limeonesha hofu yake na kufunga Operesheni zake nchini Somalia baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 22 katika pembe ya Afrika.
 

Kufungwa kwa Operesheni za MSF ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Somalia, zitaathiri maelfu ya Raia wa Somalia.
 

MSF imetoa lawama kwa makundi ya Watu wenye silaha ambao wamekuwa wakiunga mkono na kupuuzia vitendo vya mauaji, utekaji nyara na unyanyasaji wa Wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kibinaadam.