Côte d’Ivoire-Spika wa Bunge

Spika wa Bunge la Côte d’Ivoire Guillaume Soro atamatisha ziara yake katika mikoa mbalimbali nchini humo

Spika wa Bunge la  Côte d’Ivoire Guillaume Soro
Spika wa Bunge la Côte d’Ivoire Guillaume Soro

Spika wa bunge la Cote d'ivoire Guillaume Soro amehitimisha ziara yake leo jumamosi Agosti 17 katika Mkoa wa Gnanoa, baada ya kuzuru mkoa jana mikoa ya Gnaliepa, Mama na Kpokorobo ikiwa ni mkoa anakotokas mama wa raia wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo ambaye anaeshi uhamishoni nchini Ghana.

Matangazo ya kibiashara

Mikoa hiyo ndiko wanakotoka Rais Laurent Gbagbo ambaye anazuiliwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, pamoja na Charles Blegude kiongozi wa vijana wa chama cha zamani cha FPI na ambaye anazuiliwa jijini Abidjan.

Ziara hiyo ya Guillaume Soro imepokelewa na hisia tofauti katika vijiji hivyo ambapo ewashauri wake walikuwa wamemshauri kusitisha ziara yake baada ya wafuasi wa chama cha FPI kuishutumu ziara hiyo.

Spika huyo amesema hakuna mji aidha mkoa mali ya mtu binafsi, na kwamba hakukurupuka kuzuru mikoa hiyo na wala hailengi kufanya uchochezi, amesisitiza kwamba ziara yake ameifanya baada ya viongozi wa jadi kumtaka azuru eneo hilo.

Akiwa katika eneo hilo Guillaume Soro amesema yeye ndiye aliye okowa maisha ya rais Gbagbo wakati alipokamatwa April 11 wakati wa kuanguka kwa utawala wake.

Wananchi wengi wa eneo hilo wamekuwa wakilaumu hakuna maridhiano ya ukweli kwani kuna baadhi ya viongozi ambao wapo korokoroni na wengine wakizuiliwa hata kutembelewa na ndugu wa karibu wa familia.