DRCONGO-MONUSCO

Watoto zaidi ya 80 warejeshwa katika familia zao huko DRCongo kutoka mikononi mwa kundi la waasi wa Ba Kata Katanga

Mkoa wa Katanga, Kusini mwa DRCongo
Mkoa wa Katanga, Kusini mwa DRCongo RFI

Takriban watoto thamanini waliochini ya umri wa miaka minane ambao walikuwa wameajiriwa kwa nguvu katika kundi la waasi wa Bakata-Katanga katika Mkoa wa Katanga mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamerejeshwa katika familia zao. Umoja wa Mataifa nchini DRCongo MONUSCO umepongeza hatuwa hiyo muhimu ya kuwaondowa watoto 82 katika kundi la Mai-Mai Bakata Katanga wakiwemo wasichana 13.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Monusco umri wa watoto hao ni kati ya miaka minane na kumi na saba na ambao wanashukiwa kuwa waliajiriwa katika kundi hilo katika kipindi cha miezi sita iliopita.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Martin Koblee amesema wanajihusisha zaidi na taarifa za kuwepo harakati za kuwaajiri kwa nguvu watoto wadogo katika makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo na kufahamisha kuwa kitendo hicho ni uhalifu wa kivita.

MONUSCO inaamini kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, watoto 163, ikiwa ni pamoja na wasichana 22, walitenganishwa na kundi la  Mai Mai Bakata Katanga na MONUSCO na washirika wanaofanya kazi katika eneo la ulinzi wa mtoto.

Katanga, ni mkoa anakotoka rais wa DRCongo Joseph Kabila, ni mara kwa mara unaotikiswa na matokeo ya kutaka mjitengo na DRCongo.

Mwezi Julai 1960, wiki chache baada ya uhuru wa Kongo kutoka Ubelgiji, Moise Tshombe alikuwa alitangaza uhuru wa jimbo hilo tajiri, na kulazimisha Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Kwa miezi kadhaa, jimbo kuu la mkoa wa kiuchumi wa DRCongo, umekuwa ukitikiswa na machafuko ya kuongozwa na wa separatist Bakata Katanga, ambao wanalalamika juu ya usambazaji wa usawa wa utajiri baina ya kaskazini na kusini na, ambapo makampuni mengi ya kigeni yamekuwa yakifanya kazi katika jimbo hilo.

Mwezi Machi, Bakata Katanga au Kata Katanga waliendesha shambulizi na kufika hadi Lubumbashi, katika mji mkuu wa mkoa.