Afrika kusini-Migomo

Hofu ya kufanyika migomo ya wafanyakazi wa migodini na wale wa viwandani yazidi kutanda nchini Afrika Kusini

Mgomo wa wafanyakazi wa viwandani nchini Afrika Kusini
Mgomo wa wafanyakazi wa viwandani nchini Afrika Kusini

Zaidi ya wafanyakazi elfu 30 wa kweye migodi nchini Afrika Kusini hapo jana waligoma kufanya kazi kwa saa kadhaa kupinga hatua iliyotangazwa na uongozi wa mgodi wa Amplant kutaka kupunguza zaidi ya wafanyakazi elfu 6 ifikapo septemba Mosi mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Hofu ya kufanyika mgomo mkubwa wa wafanyakazi wa mgodini na wale wa viwandani inazidi kutanda wakati huu ambapo taifa hilo likijaribu kumaliza mizozo ya kwenye migodi hali ambayo inatishia ukuaji wa uchumi wa Afrika Kusini.

Mbali na wafanyakazi wa mgodini, hapo jana pia maelfu ya wafanyakazi wa viwanda vya magari nao waliandamana kwenye mji wa Port Elizabeth kushinikiza viwanda vya magari nchini humo kuwaongeza mshahara kwa asilimia 14.

Maandamano hayo yanakuja baada ya majadiliano kutafuta muafaka juu ya nyongeza ya mshahara kukwama, hali ambayo inadhohofisha harakati za uzalishaji nchini Afrika Kusini.
Mpumzi Matungo, muweka hazina wa shirika linalotetea za wafanyakazi NUMSA amesema mgomo unaendelea, na sasa wanapanga mbinu za kushinikiza zaidi serikali na kuhamasisha wafanyakazi kuhusu hatuo hiyo ya kutetea haki zao.

Wafanyakazi na waajiri wameshindwa kuafikiana baada ya wafanyakazi kuomba nyongeza ya mshahara ya asilimia 14 wakati waajiri wao wakitowa asilimia 8, mvutano huo ndio unaosababisha kuendelea kwa mgomo.

Ma mia ya wafanyakazi wameonekana jana wakiandamana mbele ya kiwanda kinachotengeza gari cha Ford de Mamelodi katika viunga vya mji mkuu wa Afrika Kusini Pretoria.

Kufuatia mgomo huu Afrika Kusini ambayo ni ya kwanza barani Afrika katika utengenezaji wa magari, kwa siku inapoteza takriban Randi milioni mia sita, sawa na dola za Marekani milioni Arobaini na tano zinazo lingana na gari elfu tatu.

Kampuni saba zinazo zalisha magari nchini humo zinajaribu mbinu zote kuhakikisha kazi inarejea kama kawaida ili kurejesha idadi ya thamani ya magari iliopotea wakati wa mgomo ili kukidhi mahitaji ya wateja wa kimataifa.