SUDANI KUSINI

Jenerali James Otong Riek kiongozi wa juu wa jeshi la nchini Sudani Kusini atiwa nguvuni kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu

Jeshi la Sudani Kusini SPLA katika moja ya operesheni zake
Jeshi la Sudani Kusini SPLA katika moja ya operesheni zake

Rais wa Sudani kusini Salva Kiir ameamuru kukamatwa mara moja kwa Kiongozi wa juu wa jeshi nchini humo, Jenarali James Otong Riek anaetuhumiwa kuendesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo lenye mgogoro la Joglei ambako jeshi la serikali linapambana na kundi la waasi.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi nchini Sudani Kusini Philip Aguer amesema Jenerali James Otong Riek, amekamatwa na maofisa usalama nchini humo baada ya ripoti iliomuhusisha na uporaji pamoja na mauaji na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Pibor

Jenerali Riek ambaye alikuwa kiongozi vikosi vya mji wa Jonglei anatuhumiwa kuamrisha wanajeshi wake kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji wananchi wa eneo hilo ambalo limekumbwa na machafuko kutokana na mapigano ya kikabila.

Makosa aliyo yatenda kiongozi huyo hayakuwekwa bayana, lakini alikuwa anaongoza kampeni inayo kosolewa ya upokonyaji silaha kwa nguvu. Mashirika yanayo tetea haki za binadamu, kampnei hiyo ilitowa fursa kwa wanajeshi wa Sudani kusini kutekeleza uhalifu wa kivita, kama vile ubakaji, uporaji na utesaji.

Jeshi la Sudani Kusini linatuhumiwa pia kuegemea upande wa jamii ya lou Nuer katika mapigani yao na watu wa jamii ya Murle, makabila ambayo yamekuwa yakipambana mara kadhaa tangu mwaka 2011 na kusababisha ma mia na hata ma elfu ya watu kupoteza maisha.

Zaidi ya watu laki tatu wamepoteza maisha katika mapigano hayo huku wengine laki moja wakiyatoroka makwao wakati wa vita vya hivi karibuni mwezi uliopita wa Julay wakati watu wa kabila la Lou Nuer waliposhambulia mji wa Pibor unaokaliwa na raia wengi wa kabila la Murle.