MISRI

Kesi ya Hosni Mubarak kusikilizwa kwa mara ya pili leo Jumapili mjini Cairo

rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak
rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak redstatements.com

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak anarejea mahakamani leo Jumapili kukabiliana na mashataka ya kuhusika katika vifo vya waandamanaji, huku viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood wakifika mahakamani kwa mara ya kwanza kwa mashtaka ya aina hiyo lakini yasiyofanana.

Matangazo ya kibiashara

Kusikilizwa kwa kesi hizo mbili katika maeneo tofauti ya mji mkuu kunafanyika katikahali ya kupambana na kuongezeka kwa mvutano unaoendelea katika nchi hiyo, ambayo imekuwa inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa tangu jeshi kumpindua rais Mohamed Morsi katika mapinduzi ya Julai 3.

Mubarak, ambaye aliondoka gerezani kwa mapumziko nyumbani juma hili,amepangiwa kufika mahakamani ambapo kesi yake itasikilizwa kwa mara ya pili katika ya madai ya kula njama katika vifo vya waandamanaji wakati wa maandamano ya mwaka 2011 ambayo yalimlazimisha kujiuzulu.