MISRI

Mahakama nichini Misri yaagiza kufungwa vituo vinne vya Televisheni

Mahakama moja mjini Cairo hii leo imeagiza kufungwa kwa vituo vinne vya Televisheni vikiwemo vile vya kimataifa na vya ndani.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili la mahakama linatolewa wakati huu ambapo waandishi wa habari wanaotumika na vyombo vya habari vya kimataifa wamejikuta matatizoni na vyombo vya usalama vya Misri ambavyo vinawashikilia baadhi yao.

Hii leo mahakama ya mjini Cairo imeagiza kufungwa kwa vituo vinne vya televisheni kikiwemo kituo cha kiarabu cha Al-Jazeera Misri, Al-Yarmuk, Al-Quds na kile cha Ahrar 25 ambacho kinamilikiwa na chama cha kiislamu cha Muslim Brotherhood.

Uamuzi huu wa mahakama unatolewa huku tayari kituo kingine cha kiislamu cha Al-Yarmuk kikiwa kimefungwa hapo juzi baada ya kutangaza habari ambayo mamlaka nchini Misri inasema ililenga kuchochea machafuko kati ya waislamu na waumini wa kikristo wa madhehebu ya Coptic.

Polisi nchini Misri wanavituhumu vituo hivyo kwa kuripoti habari za uongo pamoja na kuegemea upande mmoja wa chama cha Muslim Brotherhood haloi iliyochangia machafuko zaidi nchini humo.