SOMALIA

Rais wa Somalia anusurika baada ya msafara wake kushambuliwa na Al Shabab

Serikali ya Somalia imesema kuwa Rais wa nchi hiyo Hassan Sheikh Mohamud yuko salama baada ya kufanikiwa kumbia kufuatia shambulizi lililokua limelenga msafara wake.

Reuters/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

 

Vyamnzo vya habari vya kidiplomasia vilivyozungumza na ujumbe wa rais vimesema kuwa rais na wajumbe wake katika msafara huo wako salama na walifanikiwa kufika salama katika bandari ya Merka baada ya kufanyika kwa shambulizi hilo la kushtukiza.

Radio ya Taifa la Somalia imetangaza kuwa shambulio hilo la kushitukiza linadaiwa kufanywa na kundi la Al Shabab linalohusiana na kundi la kigaidi la Al Qaeda limedai kutekeleza shambulizi hilo.

Kundi la Al Shabab limedai kuwa lilishambulia msafara wa Rais Hassan Sheikh Mohamud na kusababisha uharibifu wa maghari yaliyokua kwenye msafara kwa kutumia makombora ya kurushwa kwa roketi.

Msemaji wa kundi la Al Shabab Abdulaziz Abu Musab amethibiosha kuwa walifanya shambulizi hilo la kushitukiza lililotokea katika eneo la Buffow karibu na badari ya Merka eneo ambalo ni ngome kubwa ya zamani ya Al Shabab.

Akisafiri nje ya Mogadishu rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud kwa kawaida husindikizwa na askalri wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika walioko nchini Somalia.

Serikali imesema mpaka sasa hakuna taarifa za majeruhi katika msafara huo ulishambuliwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabab linalohusishwa na Al Qaeda.

Zaidi ya tukio hilo la kushambuliwa Rais Mohamud, Mwezi May mwaka 2012 wapiganaji wa Al Shabab walishambulia msafara wa Rais mtangulizi wake Sheikh Sharif Sheikh Ahmed.