DRC-M23

Upinzani watishia kususia mjadala wa kitaifa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo

Siku chache kabla ya kuanzishwa kwa mchakato wa majadiliano ya kitaifa nchini DRC kama ilivyo agizwa na rais wa taifa hilo tangu mwanzzoni mwa mwaka huu, wanasiasa nchini humo wanatofautina kuhusu mazungumzo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Mkanganyiko umeibuka katika chama kikuu cha upinzani cha UDPS baada ya chama hicho kutangaza kwamba hakitoshiriki majadiliano hayo, huku wabunge kutoka chama hicho wakiona umuhimu na kutangaza kuwa watashiriki.

Chama ch MLC cha Jean Pierre Bemba Gombo alieko Hegue nacho kinasema licha ya mkanganyiko uliopo, kitashiriki kwenye mazungumzo hayo ambayo katibu wake mkuu Thomas Luhaka anasema yana umuhimu wake.

Upande wake Spika wa bunge la DRCongo Aubin Minaku anasema kuna umuhimu mkubwa wananchi wa Congo kuketi pamoja na kujadiliana kuhusu mustakabali wa taifa lao.

Hayo yanajiri wakati waasi wa M23 wakisogeza nyuma wapiganaji wake kutoka katika uwanja wa mapambano huko Goma ingawaje hali bado ni ya wasiwasi huku shughuli za kiuchumi zikidorora.

Aidha hali katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini, Kivu Kaskazini kwa kiasi fulani imerejea kuwa shwari kama ilivyokua kabla ya kuanza kwa makabiliano.