NIGERIA-BOKO HARAM

Wanamgambo 50 wa Boko Haram wauwawa na jeshi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Baadhi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria
Baadhi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria Reuters

Jeshi nchini Nigeria limesema kuwa limewaua wanamgambo hamsini wa kundi la Boko Haram kwenye operesheni iliyozinduliwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo katika kukabiliana na mashambulizi ya waasi, katika vurugu za karibuni kulikumba eneo hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanatoka katika madhehebu ya kiislam yenye vurugu walifyatua risasi kwenye soko siku ya Alhamisi katika mji wa Gajiran, na kuua watu 15, wakazi wamesema.

Kijeshi lilituma vikosi vya askari katika kukabiliana na azma ya washambuliaji ambapo kwa msaada wa vikosi vya anga waliweza kushambulia kambi za wanamgambo hao na kufanikiwa kuwaua hamsini msemaji wa jeshi Sagir Musa amewaambia waandishi wa habari mjini Maiduguri.

Mgogoro wa Boko Haram unakadiriwa kugharimu maisha ya zaidi ya watu 3,600 tangu mwaka 2009, ikiwa ni pamoja na mauaji yaliyotekelezwa na askari wa vikosi vya usalama, ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.