RWANDA-UCHAGUZI

Wananchi wa Rwanda wapiga kura kuwachaguwa wabunge kwa muhula mwingine wa miaka mitano

wananchi wa Rwanda wakipanga foleni wakati wa zoezi la upigaji kura
wananchi wa Rwanda wakipanga foleni wakati wa zoezi la upigaji kura

Raia wa Rwanda hii leo wameanza kupiga kura kuwachaguwa wabunge katika uchaguzi ambao unaendeleza utawala wa chama madarakani cha FPR cha rais Paul Kagame madarakani tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbri mwaka 1994.Takriban vituo elfu kumi na tano vimefunguliwa nchi nzima tangu mapema leo asubuhi na vinatarajiwa kufungwa baadaye jioni saa kumi, vikipambwa kwa rangi ya njano, kijani na blue rangi ya benfera ya nchi hiyo. Takriban wananchi milioni sita wanashiriki katika uchaguzi huo ili kuamuwa kutowa nafasi ya wabunge 410 waliogawanyika katika makundi manne wakiwemo pia wagombea huru.Mengi zaidi ni katika ripoti hii ya muandishi wetu wa kigali nchini Rwanda Bryason Bichwa