Mali-Kidal

Wapiganaji wa kundi la Tuareg kaskazini mwa Mali watishia kujihami iwapo jeshi litawashambulia tena

wapiganaji waasi wa kundi la MNLA kaskazini mwa Mali
wapiganaji waasi wa kundi la MNLA kaskazini mwa Mali

Waasi wa kundi la Tuareg kaskazini mwa Mali wamesema kwamba wapiganaji wao watajihami kikamilifu na wametishia kuwasambaratisha wanajeshi wa Mali iwapo watafanya tena mashambulizi mengine. Hayo ni katika taarifa iliotolewa na msemaji wa kundi la MNLA Mossa Ag Attaher baada ya kushuhudiwa mashambulizi makubwa juma lililopita kati ya wapiganaji wa kundi hilo na jeshi la Mali na kusababisha mauaji makubwa ikiwa ni mara ya kwanza kutokea kwa tukio hilo tangu kusainiwa mkataba wa amani mwezi Juni mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo serikali ya Bamako haikulipa uzito tukio hili na kulichukulia kama la kawaida ambapo jeshi la serikali lilipamabana na majambazi wenye silaha katika opresheni yao ya usalama wakati nchi hiyo ikielekea kujizatiti katika eneo la kaskazini lililokuwa chini ya mikono ya waasi wa Tuareg na wale wa makundi ya jihadi.

Uongozi wa kijeshi wa kundi hilo umetowa amri kwa wapiganaji wote wa kundi hilo waliopo katika eneo la kaskazini kujibu mashambulizi na kujihami kikamilifu iwapo watashambuliwa na kuhakikisha wamewasambaratisha wanajeshi wa serikali ya Bamako.

Msemaji wa kundi la MNLA amelaani vikali mashambulizi ya juma lililopita na kuyaita kuwa ni uvunjifu wa mkataba wa kusitisha mapigano ambapo serikali ya Bamako imeshindwa kuheshimu na kwamba hawatokubali ukatili unaofanyw a na wanajeshi wa Mali dhidi ya raia wenye asili ya kitureg.

Mossa Ag Attaher amesema kuwa wanasubiri viongozi wapya wa Mali kutowa muelekea ulio wazi na chanya kuhusu nia thabiti ya kuendeleza majadiliano juu ya kufikia hatuwa za kisheria na kisiasa kuhusu eneo la Azaward katika muda uliokubaliw akwenye mkataba wa amani uliosainiwa mjini Ouagadoudgou.

Mbali na hivo amesema kundi hilo la MNLA litachukuwa jukumu lake la kulinda maslahi ya wananchi wa eneo la Azaward wakitumia njia zote.

Kundi la MNLA na lile la HCUA ambalo pua ni kundi la waasi wa Tuareg walifikia kwenye mkataba wa amani na serikali ya Bamako Juni 18 mjini Bamako, mkataba ambao uliruhusu kufanyika kwa uchaguzi wa Julay 28 katika mji wa Kidal, kaskazini mwa Mali, ambao ulikuwa chini ya udhibiti wa makundi ya kijeshi ya Touareg baada ya operesheni ya vikosi vya Ufaransa vilivyo yafurusha makundi ya jihadi yanayofungamana na kundi la kigaidi la Alqaida katika eneo la Maghreb la Aqmi.

Mkataba huo, unaagiza usitishwaji mapigano, kurejea hatuwa kwa hatuwa kwa wanajeshi wa Mali mjini Kidal na kukusanywa katika eneo maalum kwa wapiganaji waasi.