NIGERIA-BOKO HARAM

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram wakamatwa na kundi la vijana na kukabidhiwa jeshi nchini Nigeria

Watu 11 wanaoshukiwa kuwa Wafuasi wa kundi la Wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wamekamatwa na makundi ya vijana waliojitolea kupambana na Wanamgambo hao na kisha kuwakabidhi wanajeshi wa nchini Nigeria, Kamanda wa Jeshi katika eneo hilo ameeleza na kuthibitisha kuwa Watu wannne kati yao wamepoteza maisha wakiwa kizuizini.

wapiganaji wa kundi la Boko Haram
wapiganaji wa kundi la Boko Haram
Matangazo ya kibiashara

Luteni Kanali Beyidi Martins amelipongeza kundi hilo la vijana ambao wanaasili ya mji wa Maiduguri mji mkuu wa jimbo la Borno jirani na Adamawa ngome ya Boko Haram wenye kujihami kwa mapanga na marungu.

Vijana hao walitoka Maiduguri kuelekea Michika wakiwafuata watuhumiwa hao wa ugaidi wa kundi la Boko Haram na kufaanikiwa wakiwa pamoja na watu watano waliowapa hifadhi na walitukabidhi, amesema kanali Beyidi Martins.

Washukiwa wanne walipoteza maisha siku ya Jumamosi na Jumapili katika majengo ya jeshi kufuatia majeraha walioyapata wakati wa kukamatwa kwao.

Jimbo la Borno ndiko kuliko ngome ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram ambapo limezidisha hujuma katika kipindi cha miezi mitatu iliopita mashambulizi dhidi ya makundi ya vijana wanaojihami na ambao wamekuwa wakipewa mafunzo na kupongezwa na jeshi.

Vinaja wa makundi hayo yakujihami wamefaulu kuwafurusha wapiganaji wa Boko haram katika mji wa Maiduguri na kuwapeleka hadi mpakani mwa Cameroon, Tchad na Niger.

Kundi hilo la Boko Haram limekuwa likidai uundwa wa taifa la kiislam kaskazini mwa Nigeria ambapo mapambano yamekwisha dumu sasa miaka minne. Tangu mwanzoni mwa mwezi Mei, jeshi limekuwa likiendesha operesheni katika maeneo yaliotangazwa hali ya hatari ili kukomesha uasi huo.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch Machafuko ya kundi la Boko Haram yamesababisha zaidi ya watu elfu tatu na mia sita kupoteza maisha tangu mwaka 2009