KENYA-RUTO-ICC

Kesi ya naibu wa rais nchini Kenya William Ruto kusikilizwa tena leo kwenye mhakama ya uhalifu wa kivita ya ICC

Naibu wa rais nchini Kenya William Ruto akiwa na mawakili wake
Naibu wa rais nchini Kenya William Ruto akiwa na mawakili wake

Kesi ya naibu wa rais nchini Kenya William Ruto na mwanahabari Joshua Sang inasikilizwa tena leo kwenye mahakama ya  uhalifu wa kivita ya ICC ilioko mjini Hague nchini Uholanzi. Wawili hao wanatuhumiwa kuhusika katika kufadhili na uchochezi wa mauaji yaliotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Shahidi wa kwanza anatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya mahakama hiyo.Muandishi wetu Paulo Silva ana mengi kutoka jijini nairobi