UFARANSA-CAIRO

Raia mmoja wa Ufaransa uawa katika jela moja jijini Cairo baada ya kupewa kipigo na wagunwa wenziye

Raia mmoja wa Ufaransa ameuawa akiwa jela baada ya kupigwa vikali na wafungwa wenzake katika jela moja jiji Cairo. Raia huyo wa Ufaransa alikamatwa juma moja lililopita katika kata ya Zamalek kwa tuhuma za kuvunja amri ya kutotembea usiku na ambapo alikutwa mlevi na kupelekwa moja kwa moja katika jela la Qasr el-Nil mjini kati.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ufaransa alietambulika kama mwalimu ambaye baadaye aliwekwa korokoroni baada ya kukamatwa kwek na kuendeshewa kipigo na wafungwa wenziye waliomjeruhi. Raia huyo  alifariki kutokana na majeraha aliyo yapata.

Washukiwa sita ambao walikamatwa pamoja na raia huyo wa Ufaransa wanahojiwa wakati huu na vyombo vya usalama katika kuendesha uchunguzi juu ya kipigo kilicho sababisha kifo.

Uchunguzi unaonyesha kuwa kifo cha raia huyo kimesababishwa na kuvuja damu kwa ndani na kipigo alichopata kwa kupigwa kitu chenye uzito kichwani.

Duru za kiusalama zimearifu kuwa wakati wa kukamatwa kwake raia huyo alikuwa hana visa. Ubalozi wa Ufaransa jijini Cairo umesema raia huyo alikuwa anaeshi jijini Cairo tangu kipindi kirefu.